Mnyika kutoshiriki kusaini mikataba ya uchaguzi

 

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. John Mnyika kupitia mtandao wa X amesema kuwa hatashiriki kwenye kikao cha kusaini Kanuni ya Maadili ya Uchaguzi kwa mwaka 2025, kinachofanyika leo katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jijini Dodoma.

Amesema kuwa ndiye mwenye mamlaka ya kisheria kusaini kwa niaba ya chama, na hajamteua kiongozi au afisa yeyote kuwakilisha CHADEMA kwenye kikao hicho.

Kauli hiyo inakuja baada ya Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Ramadhan kusema kuwa chama cha siasa ambacho hakitasaini maadili hayo hakitaruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo.


Post a Comment

Previous Post Next Post