Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme (Tanesco), Mhandisi Gissima Nyamohanga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika ajali ya gari katika Wilaya ya Bunda, mkoani Mara.
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mara, Nickison Babu amenukuliwa na vyombo vya habari akithibitisha kutokea kwa ajali na kifo cha Nyamohanga.
Amesema mwili wake mpaka sasa upo hospital ya DDH wilayani humo.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni dereva gari dogo aina Land Cruiser alijaribu kumkwepa muendesha baiskeli na kwenda kugongana na lori ambapo katika ajali hiyo, dereva wa gari la mkurugenzi nae amefariki dunia.

Post a Comment