Kocha wa zamani Madrid afariki dunia

Kocha wa zamani wa Real Madrid Leo Beenhakker amefariki akiwa na umri wa miaka 82, klabu hiyo ya Uhispania imesema.

Mholanzi huyo aliiongoza klabu hiyo kati ya 1986 na 1989, na tena mwaka 1992.

Alishinda mataji sita katika misimu yake minne akiwa Real Madrid, ikiwa ni pamoja na mataji matatu mfululizo ya LaLiga kati ya 1987 na 1989.

“Real Madrid ingependa kutoa rambirambi na upendo kwa familia yake, vilabu na wapenzi wake,” klabu hiyo ilisema katika taarifa yake.


 

Post a Comment

Previous Post Next Post