Kimbunga Chido kimeua watu 94 nchini Msumbiji tangu kilipotua katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki wiki iliyopita, mamlaka za ndani zimesema.
Taasisi ya Kitaifa ya Kudhibiti Hatari na Majanga nchini humo (INGD) imesema watu 768 walijeruhiwa na zaidi ya watu 622,000 wameathiriwa na maafa hayo.
Chido kiliikumba Msumbiji tarehe 15 Desemba kwa upepo wa kasi ya kilomita 260 kwa saa (160mph) na 250mm za mvua katika saa 24 za kwanza.

Kimbunga hicho kilisababisha maafa kwa mara ya kwanza katika eneo la Bahari ya Hindi la Ufaransa katika visiwa Mayotte, kabla ya kuhamia Msumbiji, Malawi na Zimbabwe.

Post a Comment